Jumapili, 6 Aprili 2014


Sunday, April 6, 2014

MCHUNGAJI AFUMANIWA NA WANAWAKE WATATU GESTI

Stori: Richard Bukos na Issa Mnally  

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.


 OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR
Ilikuwa Jumanne ya Aprili Mosi, 2014, saa 4:14 asubuhi, chanzo cha habari kilipiga simu chumba cha habari cha Global na kuwataka makachero wa OFM ambapo alipounganishwa nao alisema:
“Jamani kama kweli hapo ni OFM nina malalamiko. Mimi nimeshtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na pastor (mchungaji) mmoja anaitwa Rubanguka.



“Huyu pastor amempa dili dada mmoja kumtafutia wasichana wazuri watatu na kuwapeleka kwenye nyumba moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake huku wao wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo. Wasichana wameshapatikana.”

MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUU
Mtoa habari huyo aliendelea kudai kuwa, pastor huyo alisema wasichana watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia usaili wa kwenda kuwauza kwenye kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye ni wakala wa kuwapelekea malaya huko.




Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi wanawake hao kitita cha shilingi 300,000 kila mmoja kwa wale watakaofaulu kumchezea vizuri, sanjari na kuwakatia hati za kusafiria ‘passport’.


 OFM YAWEKA MTEGO
Baada ya kupata ishu nzima, OFM ilifanya ukachero na kugundua mahali ambapo tukio hilo lilipangwa kufanyika, ni kwenye danguro moja lililopo Kinondoni jijini Dar.



 OFM ilifika kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu wake ambapo walifanikiwa kuweka mitambo yao sambamba na kulishirikisha jeshi la polisi kwa ajili ya kumnasa mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo hivyo.
 

Saa 8:11 mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo waliwashuhudia warembo watatu, weupe wakielekea kwenye nyumba ambayo mtoa habari wetu aliielekeza. 

Kitambulisho cha Pasta.

PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE
Saa 11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka. Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa wanawake hao.

Bango lililopo Kinondoni Mkwajuni, Dar likieleza lilipo kanisa la Pasta huyo.
 MCHEZO WAANZA
Saa 11:40 jioni, makachero wa OFM walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa, tayari mchezo ulishaanza ambapo waliwataarifu polisi na kuungana nao kwenda kuvamia nyumba hiyo.

 
 Msafara wa OFM na polisi hao ulifika nje ya chumba kilichokuwa kikidaiwa kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki na wanawake waliokuwa kama wapo kwenye darasa la siri zilisikika.

 
 Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.

 
 PASTOR APATA MCHECHETO
Pasta John na wanawake hao walitii amri kwa kufungua mlango ambapo mchungaji huyo alikumbwa na mchecheto na kutaka kurukia juu ya dari lakini polisi walimtafadhalisha kutulia pamoja na wanawake hao kama walivyo.

 
 OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa wakimnengulia viuno.

 
 Baada ya kupewa kibano, warembo hao walimwanika pastor huyo kwamba ndiye aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu ili awalipe shilingi laki tatu kila mmoja, pia kuwapeleka Uarabuni kwenye kasino.

 
 UTETEZI WA PASTOR
Kwa upande wake, Pastor John alijitetea kuwa anaomba asamehewe kwa gharama zozote ili taarifa hizo zisifike popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri yake bali shetani alimpitia.

 
 “Jamani naomba tumalize humuhumu ndani, mnajua mimi ni Pastor wa Kanisa la Maximum Deliverance, sasa ukweli ni kwamba waumini wangu hawatanielewa, chondechonde ilindieni kazi yangu jamani,” alijitetea.

 
 Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio, pastor huyo na wanawake ‘wake’ walikuwa kwenye harakati za kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zinazostahili.

 KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Siku zote kazi ya OFM ni kuwajibikia matendo maovu na si kuwaonea watu  kwa lengo la kuwachafua. OFM inapopata habari huichunguza ukweli wake kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kuifanyia kazi moja kwa moja, yaani kufika kwenye eneo la tukio.


 Lengo kubwa la kutoa habari za aina hii ni kuwakumbusha watu namna ya kuishi maisha yanayompendeza  Mungu. Wengi wamebadilika, sasa wanaishi vizuri wakiwa watu wapya na wanyenyekevu pia wenye kufundisha wenzao.


Credit: GPL

TUNACHORA RAMANI ZA NYUMBA VIJIJINI NA MIJINI, ZA MATAJIRI NA MASIKINI KWA BEI POA

  TUNACHORA RAMANI ZA NYUMBA ZA WATU BINAFSI, VIJIJINI NA MIJINI, MASHIRIKA, TAASISI NA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI.

DUNIA NI SASA, MAKAZI BORA VIJIJINI NA MIJINI NI KUANZIA SASA.

HATA NYUMBA YA VYUMBA VITATU INACHORWA, USIOGOPE KUJARIBU.
 
 UTAKACHOTAKIWA KUFANYA, UTATOA WAZO NYUMBA YAKO UNAVYOTAKA IWE, UTACHOREWA

WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0754 440749/0655 440749 TUKUUNGANISHE NA WATAALAM KWA BEI POA KULINGANA NA UHITAJI WA NYUMBA UNAYOIHITAJI.

NEWS.....WANAFUNZI SITA TU WAMERIPOTI SEKONDARI KATI YA 27 WALIOFAULU

Ni huko Mbarali Mbeya

SOMA HOJA YA MTIKILA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA ANAVYOTAKA MCHAKATO USITISHWE.....





HOJA MAALUM
MCHAKATO WA KATIBA MPYA USITISHWE
(ILI UANZE UPYA KWA USAHIHI)

Waheshimiwa Wajumbe, huu ni ushauri wa kizalendo kwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kwamba mchakato mzima wa Katiba mpya ubatilishwe pamoja na Rasimu ya Katiba, kwa misingi ifuatayo: KIGEZO CHA KWANZA Mchakato wa Katiba halali ya wananchi lazima uanze na uelimishaji wa wananchi wote, kwa sababu wananchi walio wengi hawajui kabisa suala la Katiba, kiasi cha wengine kudhani katiba ni aina fulani ya mboga, wakati ni jambo la msingi wa Taifa lolote duniani linalomhitaji kila mwananchi ashiriki, kama inavyoagiza Ibara ya 21(2) ya Katiba yetu iliyopo, kwamba ni haki ya kila raia kushiriki kwa ukamilifu. 

 Katiba ya Nchi ni lazima itokane na makubaliano ya raia wote, tena kutokana na uelewa sahihi wa kila mmoja wao. Ndiyo maana hatua ya kwanza na muhimu kuliko zote ya kutengeneza Katiba ya Nchi ni uelimishaji makini wa familia yote, zoezi ambalo linaweza kuchukua miaka, kama wenzetu wa Kenya walivyotumia takriban miaka mitatu kuelimisha umma wao ingawa uliokuwa na ufahamu kuliko umma wetu. 

Ni dhahiri kwamba hata ukusanyaji wa maoni uliofanyika hauna uhalali, kwa sababu yalichukuliwa maoni ya katabaka ka wananchi wachache sana wenye uelewa. Haijalishi hata kama hao waelewa wachache walitoa maoni mazuri yakatengenezewa Rasimu hii, Katiba inamtaka kila raia aeleweshwe vizuri ili ashiriki kwa ukamilifu

Ni usanii kusema wanakusanya maoni ya watu, wakati watoaji wa maoni wametegewa sheria kandamizi kama za “Uchochezi’’ ili wasizungumzie machafu ya watawala yaliyowatesa kwa miaka 53 ya uhuru, kusudi waweze kuyadhibiti vizuri katika Katiba yao. 

Ndiyo maana tulisema kwanza yafutwe yale masheria kandamizi, ili raia wakishaelimishwa kuhusu Katiba yao waweze kutoa maoni yao bila woga. Hakuna mjadala hapa, kinachotakiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Katiba, siyo matakwa ya Rais au CCM. Katiba inataka itumike HAKI sawa kuunda chombo cha haki sawa na wajibu sawa kwa nchi yetu kwetu sisi sote na vizazi vyetu vyote vijavyo. 

Mchakato wa Katiba unaoendeshwa bila uelewa na uhuru kamili wa wananchi, moja kwa moja unakuwa hauna uhalali, haijalishi hata kama mapesa mengi kiasi gani yametumika katika haramu hiyo. Haramu haiwezi kuzaa halali. 

Bunge maalum la Katiba linapaswa kuukataa. Katiba inayotokana na kugoma kuwapa ufahamu sawa wananchi wote, na kutumia maoni ya kakundi kadogo tu ka wananchi kwa kuwapuuza raia zaidi ya milioni 46 si halali, tena ni ubaguzi wa kikatili na ukiukaji wa Ibara ya 12 na ya 13 ya Katiba ya Jamhuri. Haramu haiwezi kuzaa halali. 

Ni wajibu wa Bunge maalum la Katiba kuukataa mchakato mzima wa Katiba mpya, kwa uaminifu kwa Mungu, kwa Wana wa Tanganyika na wananchi wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar. 


KIGEZO CHA PILIKusimamiwa na watawala utengenezaji wa Katiba ya wananchi, tena viongozi wa CCM isiyoficha azma yake ya kutawala juu ya wenzao milele licha ya kuchukiwa vibaya sana na wananchi, kunafuta kabisa uhalali wa mchakato mzima wa Katiba. Serikali ni kiungo kilicho ndani ya Katiba ambayo ni ya Wananchi, kama isemavyo Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri kwamba mamlaka yote ya utawala wa nchi yamo mikononi mwa wananchi wenyewe, yaani hata mamlaka ya utengenezaji wa Katiba yao wanayo wao, si ya Rais au serikali yenye kuajiriwa tu na wananchi! Kitendo cha Rais cha kuteua yeye Tume ya kukusanya Maoni bila kuwaelewesha kwanza wananchi, na kuipa yeye maelekezo, na kuilipa mapesa lukuki kama rushwa, na kuwanyangánya raia haki yao ya kuhoji juu ya uhalali wa muungano, kinapoteza uhalali wa mchakato mzima wa Katiba, Ndugu Wajumbe, kitendo cha Rais cha kuteua yeye wajumbe wa Bunge la Katiba kwa kuzingatia maslahi yake binafsi na ya chama ckake, badala ya kuwaelewesha wananchi wote vyakutosha, ili wachague wao wenyewe wajumbe wao katika Bunge maalum la Katiba yao, kutokana na kuwaamini jinsi walivyo na mzigo juu ya hatima ya nchi yao na hatima yao na watoto wao, kimelikosesha Bunge hili uhalali Bunge maalum la Katiba limekoseshwa uhalali na Rais Kikwete, kwa kupendelea wanasiasa kwa asilimia 90% na hasa wa chama chake, aliowapenyeza kwa wingi kwa kutumia taasisi za kiraia, majority ya wabunge wao katika Bunge la Muungano, Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliyojitoa katika muungano (kitendo ambacho ni matusi kwa Watanganyika), ilimradi CCM wajipatie theluthi mbili za kujipitishia maslahi yao. Katika Watanganyika milioni 48 wanasiasa wako takriban milioni 5, hivyo kwamba wananchi milioni 43 wamepuuzwa katika mchakato wa Katiba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni