Ijumaa, 4 Aprili 2014

Friday, April 4, 2014 MTENDAJI WA KIJIJI NA HALMASHAURI YA KIJIJI WATIMULIWA KIJIJI CHA IWIJI KWA UFUJAJI WA MBOLEA ZA RUZUKU Kushoto Afisa tarafa Aaron Sote akipokea funguo toka kwa mtendaji Anton Ndisa Afisa Kilimo wilaya Marselin Mlelwa atitoa takwimu za mgao wa mbolea iliyotolewa Octoba 10 mwaka jana kwa kijiji hicho baada ya kupitishwa na Kamati ya Mbolea ya Wilaya ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya. Wananchi wakifuatilia mkutano huo kwa makini Saimoni Kasebele moja kati ya wajumbe kamati ya mbolea ambayo haikufanya kazi kijijini Moja kati ya wananchi ambao waliwekwa mahabusu na mtendaji baada ya kufuatilia mgao wa mbolea Wajumbe waliotimuliwa Mbolea inayosadikiwa kuibwa Wananchi wa kijiji cha Iwiji Kata ya Iwiji wilaya ya Mbeya wamemtimua Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Kata aliyefahamika kwa jina la Anthon Ndisa kwa tuhuma za ubadhilifu wa Mbolea za ruzuku mifuko 189 iliyotolewa na serikali kwa kipindi cha msimu wa 2013/2014. Hatua hiyo imechukuliwa na wananchi hao katika mkutatano wa hadhara uliofanyika kijijni hapo ambapo Afisa Kilimo wilaya Marselin Mlelwa atitoa takwimu za mgao wa mbolea iliyotolewa Octoba 10 mwaka jana kwa kijiji hicho baada ya kupitishwa na Kamati ya Mbolea ya Wilaya ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya. Afisa Tarafa ya Isangati Aaron Sote ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ndiye alisimamia mkutano huo amesema kuwa Afisa kilimo ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa ya mgao wa mbolea kama kamati ilivyopitisha. Baada ya kufunguliwa mkutano na Mwenyekiti wa kijiji Patson Ngao Afisa Tarafa alimkaribisha Afisa Kilimo kusoma jinsi mgao wa mbolea ulivyokwenda ambapo alisema Kitongoji cha Mabula kilipata mbolea ya Dap mifuko 20 Urea 20, Kitongoji cha Iwiji Dap mifuko 8 Urea 20,Kitongoji cha Soweto mifuko 6 Dap na Urea mifuko 16. Kitongoji cha Magole kilipata Dap mifuko 6 na Urea mifuko 16,Kitongojo cha Mtukula Dap mifuko 6 na Urea mifuko 16 wakati Kitongoji cha Ntinga kilipata Dap mifuko 8 na Urea mifuko 20 wakati Kitongoji cha Vimetu kikipata Dap mifuko 7 na Urea mifuko 20. Katika mgao huo kulikuwa na upungufu wa mifuko 50 ya Dap na Urea mifuko 36 ambayo wakulima hawajapatiwa na kwamba ikifika wananchi wagawiwe ili kukamilisha idadi ya mifuko 189 kwani hivi sasa mifuko iliyogawiwa ni mifuko 139 tu. Baada ya kusomwa taarifa hiyo wananchi walitaharuki wakidai kuwa hesabu hizo zimetengezwa na Mtendaji Anthon Ndisa kwa manufaa yake kwani wananchi hawajapata mbolea hiyo licha ya kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya kupitia Afisa Pembejeo Lupakisyo Masuba. Kutokana na kutoridhishwa na taarifa hiyo na kwamba wananchi wamehujumiwa na uongozi wa kijiji kupitia viongozi wa vitongoji ambao walikiri kupokea mbolea hiyo na kuigawa wakati kuna kamati mbolea ya kijiji ambayo ndiyo ilikuwa na jukumu la kugawa ambapo uongozi wa kijiji ukidai kamati hiyo ilivunjwa. Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya pembejeo Simon Kasebele amesema kuwa kati iliyokuwa na wajumbe sita ambao ni Mwenyekit Venance Lwinga,Lucia Mose,Sara Kasalama,Patson Kayelewe na Eva Makanika haikufanya kazi kutokana na agizo la Mtendaji aliyedai kuwa kamati imevunjwa wakati siyo kweli bali ilikuwa ni njama za kuwahujumu wananchi kwa manufaa yao. Baada ya majadiliano marefu wananchi waliamua kuirudisha Kamati ya Mbolea huku wakimtaka Mtendaji kuondolewa haraka ili kuepusha ufujwaji wa mali za kijiji na kuwatimua wenyeviti wote wa vitongoji na kumwacha Mwenyekiti wa kijiji pekee Patson Ngao wakidai hahusiki na ubadhilifu kwani alizungukwa na Mtendaji kupitia wenyeviti wa vitongoji. Kwa upande wake Afisa Kilimo Marselin Mlelwa amesema taarifa ataifikisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ili kutoa maamuzi kwa vile Mtendaji ni Mwajiriwa hivyo lazima taratibu za utumishi lazima zifuatwe. Ili kuhakikisha hakuna nyaraka zozote zinachukuliwa Ofisi Mwenyekiti na Kamati ya Mbolea watafanyia shughuli zao katika ghala la Kijiji wakati Mtendaji aliagizwa kubaki na funguo hadi hapo Halmashauri itakapotoa taarifa zake baada ya ukaguzi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Upendo Sanga amekiri kupokea taafa za malamiko ya wananchi wa Iwiji na kuwataka kuwa na subira kwani serikali ina utaratibu wake ambao lazima ufuatwe pindi mtumishi anapotuhumiwa kwa jambo lolote ikiwa na pamoja na kuunda Tume ya Uchunguzi na Wakaguzi ili kupata Ushahidi. Uchunguzi uliofanywa baada wananchi kulalamikia utaratibu uliotumika kugawa mbolea hiyo Mtendaji wa Kijiji alirejesha mifuko 50 ya Dap ambayo imehifadhiwa kwa mmoja wa Mawakala kijijini hapo ili kuficha ushahidi na kuonekana mbolea hiyo ilikuwepo wakat ukweli ni kwamba mbolea hiyo tangu itolewe mwezi Octoba wananchi hatanufaika nayo kwa kuwa msimu wa kilimo umepita na kijiji kukabiliwa na hatari ya njaa. Mbali ya tuhuma ya Mbolea Mtendaji anatuhumiwa kufuja fedha za serikali na michango ya wananchi kwa ajili ya kituo cha Afya hivyo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri anapofanya uchunguzi wa Mbolea afanye ukaguzi pia mradi wa Kituo cha Afya na kama ikibainika Mtendaji na Halmashauri ya Kijiji wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Friday, April 4, 2014


MTENDAJI WA KIJIJI NA HALMASHAURI YA KIJIJI WATIMULIWA KIJIJI CHA IWIJI KWA UFUJAJI WA MBOLEA ZA RUZUKU


Kushoto Afisa tarafa Aaron Sote akipokea funguo toka kwa mtendaji Anton Ndisa 


Afisa
Kilimo wilaya Marselin Mlelwa atitoa takwimu  za mgao wa mbolea
iliyotolewa Octoba 10 mwaka jana kwa kijiji hicho baada ya kupitishwa na
Kamati ya Mbolea ya Wilaya ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.


Wananchi wakifuatilia mkutano huo kwa makini




Saimoni Kasebele moja kati ya wajumbe kamati ya mbolea ambayo haikufanya kazi kijijini


Moja kati ya wananchi ambao waliwekwa mahabusu na mtendaji baada ya kufuatilia mgao wa mbolea




Wajumbe waliotimuliwa




Mbolea inayosadikiwa kuibwa 
























Wananchi wa
kijiji cha Iwiji Kata ya Iwiji wilaya ya Mbeya wamemtimua Mtendaji wa Kijiji
hicho ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Kata aliyefahamika kwa jina la Anthon Ndisa
kwa tuhuma za ubadhilifu wa Mbolea za ruzuku mifuko 189 iliyotolewa na serikali
kwa kipindi cha msimu wa 2013/2014.

Hatua hiyo
imechukuliwa na wananchi hao katika mkutatano wa hadhara uliofanyika kijijni
hapo ambapo Afisa Kilimo wilaya Marselin Mlelwa atitoa takwimu  za mgao wa mbolea iliyotolewa Octoba 10
mwaka jana kwa kijiji hicho baada ya kupitishwa na Kamati ya Mbolea ya Wilaya
ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.

Afisa Tarafa
ya Isangati Aaron Sote ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ndiye alisimamia
mkutano huo amesema kuwa Afisa kilimo ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa ya
mgao wa mbolea kama kamati ilivyopitisha.

Baada ya
kufunguliwa mkutano  na Mwenyekiti
wa kijiji Patson Ngao Afisa Tarafa alimkaribisha Afisa Kilimo kusoma jinsi mgao
wa mbolea ulivyokwenda ambapo alisema Kitongoji cha Mabula kilipata mbolea ya
Dap mifuko 20 Urea 20, Kitongoji cha Iwiji Dap mifuko 8 Urea 20,Kitongoji cha
Soweto mifuko 6 Dap na Urea mifuko 16.

Kitongoji
cha Magole kilipata Dap mifuko 6 na Urea mifuko 16,Kitongojo cha Mtukula Dap
mifuko 6 na Urea mifuko 16 wakati Kitongoji cha Ntinga kilipata Dap mifuko 8 na
Urea mifuko 20 wakati Kitongoji cha Vimetu kikipata Dap mifuko 7 na Urea mifuko
20.

Katika mgao
huo kulikuwa na upungufu wa mifuko 50 ya Dap na Urea mifuko 36 ambayo wakulima
hawajapatiwa na kwamba ikifika wananchi wagawiwe ili kukamilisha idadi ya
mifuko 189 kwani hivi sasa mifuko iliyogawiwa ni mifuko 139 tu.

Baada ya
kusomwa taarifa hiyo wananchi walitaharuki wakidai kuwa hesabu hizo
zimetengezwa na Mtendaji Anthon Ndisa kwa manufaa yake kwani wananchi
hawajapata mbolea hiyo licha ya kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya kupitia
Afisa Pembejeo Lupakisyo Masuba.

Kutokana na
kutoridhishwa na taarifa hiyo na kwamba wananchi wamehujumiwa na uongozi wa
kijiji kupitia viongozi wa vitongoji ambao walikiri kupokea mbolea hiyo na
kuigawa wakati kuna kamati mbolea ya kijiji ambayo ndiyo ilikuwa na jukumu la
kugawa ambapo uongozi wa kijiji ukidai kamati hiyo ilivunjwa.

Mmoja wa
wajumbe wa Kamati ya pembejeo Simon Kasebele amesema kuwa kati iliyokuwa na
wajumbe sita ambao ni Mwenyekit Venance Lwinga,Lucia Mose,Sara Kasalama,Patson
Kayelewe na Eva Makanika haikufanya kazi kutokana na agizo la Mtendaji aliyedai
kuwa kamati imevunjwa wakati siyo kweli bali ilikuwa ni njama za kuwahujumu
wananchi kwa manufaa yao.

Baada ya
majadiliano marefu wananchi waliamua kuirudisha Kamati ya Mbolea huku wakimtaka
Mtendaji kuondolewa haraka ili kuepusha ufujwaji wa mali za kijiji na kuwatimua
wenyeviti wote wa vitongoji na kumwacha Mwenyekiti wa kijiji pekee Patson Ngao
wakidai hahusiki na ubadhilifu kwani alizungukwa na Mtendaji kupitia wenyeviti
wa vitongoji.

Kwa upande
wake Afisa Kilimo Marselin Mlelwa amesema taarifa ataifikisha kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ili kutoa maamuzi kwa vile Mtendaji ni Mwajiriwa hivyo
lazima taratibu za utumishi lazima zifuatwe.

Ili
kuhakikisha hakuna nyaraka zozote zinachukuliwa Ofisi Mwenyekiti na Kamati ya
Mbolea watafanyia shughuli zao katika ghala la Kijiji wakati Mtendaji aliagizwa
kubaki na funguo hadi hapo Halmashauri itakapotoa taarifa zake baada ya
ukaguzi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Upendo Sanga amekiri kupokea taafa za
malamiko ya wananchi wa Iwiji na kuwataka kuwa na subira kwani serikali ina
utaratibu wake ambao lazima ufuatwe pindi mtumishi anapotuhumiwa kwa jambo
lolote ikiwa na pamoja na kuunda Tume ya Uchunguzi na Wakaguzi ili kupata
Ushahidi.

Uchunguzi
uliofanywa baada wananchi kulalamikia utaratibu uliotumika kugawa mbolea hiyo
Mtendaji wa Kijiji alirejesha mifuko 50 ya Dap ambayo imehifadhiwa kwa mmoja wa
Mawakala kijijini hapo ili kuficha ushahidi na kuonekana mbolea hiyo ilikuwepo
wakat ukweli ni kwamba mbolea hiyo tangu itolewe mwezi Octoba wananchi
hatanufaika nayo kwa kuwa msimu wa kilimo umepita na kijiji kukabiliwa na
hatari ya njaa.

Mbali ya
tuhuma ya Mbolea Mtendaji anatuhumiwa kufuja fedha za serikali na michango ya
wananchi kwa ajili ya kituo cha Afya hivyo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri
anapofanya uchunguzi wa Mbolea afanye ukaguzi pia mradi wa Kituo cha Afya na
kama ikibainika Mtendaji na Halmashauri ya Kijiji wafikishwe kwenye vyombo vya
sheria.   


IMEANDALIWA NA CLEVER J.LONJE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni