KANUNI AU TABIA ZA MJASIRIAMALI
TABIA AU SIFAZA UJASIRIAMALI.
Ni tabia gani unahitaji ili upate mafanikio katika biashara au shuguri yoyote unayofanya?
ili ufanikiwe
katika shughuri au biashara unayofanya au unayotarajia kufanya ni lazima
uwe na mtazamo sahihi na mtazamo chanya. ujasiriamali una kanuni zake
amboazo ni muhimu sana ili mtu afikie mafanikio aliyoya panga,kama mtu
akishindwa kufuata kanuni hizo basi anakuwa na nafasi ndogo ya kupata
mafanikio katika shughuri yake.
KANUNI ZA UJASIRIAMALI
Tabia za ujasiriamali zinaweza
kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakini tabia
zingine hazifundishiki hizi ni
zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika
kufikili,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo
haziwezi kufundishika. Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo zinafundishika
ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika
biashara. Zifuatazo ni tabia za ujasiriamali.
1.
kuthubutu
hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa
tunazungumzia uwezo na utayali wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara
fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga
wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa
hasara,hawajui jinsi ya kuendesha amradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni
lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu
kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili
mwanasema” UWOGA NI UMASIKUNI”.
2.
Nidhamu
Hii pia ni
kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awena na nidhamu katika
biashara yake,awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na
nidhamu ya kufanya kakazi kwa bidii.nidhamu ni hanzo ch mafanikiao. Mfano
mfanyabiashara wa duka ni lazima uwe na nidhamu kwa wateja wake ili
awasimkimbie.
3.
Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa
tayari kufanya akazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya.
Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo,anatakiwa kujua soko
linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua mabadiriko yanayojitokeza
katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
4.
kuwa na uwezo wa kuongoza
mjasiriamalia
lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai
uongozi ni kalama ombayo mtu anazaliwa
nayo au anapewa na Mungu,ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha
kuongoza,lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika
ujasiliamali uongozi ni jambo muhimu sana,mjasiliamli lazima aweze kuogoza
biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa
kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu
za uogozi ili apate matunda kwaklile ambacho anafanya.
5.
Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu
kikubwa hapa ni lazima mjasiriamli awe
anaipenda kwa dhati shughuri anayofanya hii itamasahidia kufanya kazi kwa
moyo.Kama unapenda kazi unayo fanya basi kaziyo haitakuwa mgumu bali,bali
utakuwa unafanya kitu ambacho kwa ko ni hobi na mwisho wa siku utafanya kazi
kwa bidii na amaarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi.hivyo ni muhimu kuwa
na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
6.
Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni
tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,watja wengi wanapenda mtu mwamifu
na mkwali. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya
uamifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika bei zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo
itaua biashara yako.
7. Dhamira
Mtu yeyote
naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa
kutosha,kufanya kazi kwa didii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhaira. Lengo
au dhamila ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio.
Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
8. Kwenda na wakati
Mjasiriamali
lazima aende na wakati iliaweze kutambua mabadiriko mbalimbali yanayo jitokeza
katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa
nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko
huria,kwenda na wakati pia kunatoa fulsa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za
uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na
kusoma magazeti,kufanya utafiti,kurambaza katika mitandao mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni