Jumatatu, 7 Aprili 2014



PICHA ZA KOMPYUTA NA VIFAA MBALIMBALI ZA VITU VINAVYOHUSIANA NA KOMPYUTA.


Kuna aina mbalimbali za kompyuta na ambazo zina maumbo na miundo tofautitofauti.

Hapa chini kuna aina mbali mbali za picha zinazoonyesha aina mbalimbali za kompyuta hizo.


Kompyuta hizi hapa ndiyo aina mabyo watu wengi wamezoea kuziona na kuzitumia.

Hii huitwa Deski topu kompyuta/Desktop Computer.




Hii kompyuta ndogo inaitwa laputopu/laptop. Ni aina ndogo ambayo hufaa kubeba na kutembea nayo sehemu mbalimbali.





Vifaa Vikuu

Kuna aina kuu tano za vifaa vumikavyo katika kompyuta:


  1. Vifaa vya kuingiza:
    [input devices]

    Vifaa vya kuingiza ni vifaa atumiavyo mtumiaji kuwasiliana/kuongea na kompyuta unayotumia.Hapa chini kuna picha na maelezo mafupi juu ya vifaa hivyo;

    (1): Kiibodi [keyboard]:


    Hiki ni kifaa kitumikacho kwa kuandikia. Kupitia hiki kifaa mtumiaji huweza kupata herufi zote na namba kwa mpangilio wa kiitaalamu ambao humfanya aweze kuandika kazi zake.



      Pia kuna baadhi ya vitufe muhimu ambavyo inapaswa mtumiaji wa kompyuta anapaswa avifahamu ili kuweza kuafanya kazi yake bila mkwaruzo.
      1. Cha kwanza ni SPACE-BAR hiki kinapatika kwenye kiibodi yako kwenye vitufe vya upande katikati juu . Hiki kitufe kazi yake ni kufuta kwa hatua kwa kurudi nyuma.


      2. Upande wako wa kushoto kwenye vitufe vilivyoko mwishoni kuna kitufe kingine kilichoandikwa CAPS LOCK .

        Hiki kitufe kazi yake ni kubadilisha maandishi toka herufi ndogo kwenda kwenye herufi kubwa na kinyume chake.


      3. Kitufe kingine ni kile kilichopo upande wa kushoto pia chini ya kile cha caps lock . Hiki kinaitwa SHIFT

        hiki kinweza kutumika pia kubadilisha herufi kubwa na ndogo vilevile ila unapaswa kukishikilia wakati unapobadilisha. Shift zipo mbili moja upande wa kushoto na nyingine katikati ila zote zinafanya kazi sawa.


      4. Upande wa katikati kuna kitufe kingine kinachoitwa DELETE

        hiki kazi yake ni kufuta maandishi yote yale ambayo utakuwa umeyachagua.


      5. Sehemu ya kati ya kiibodi yako pamoja na upande wa kulia wa kiibodi yako chini kuna vitufe vilivyoandikwa ENTER.

        Hivi vitufe kazi yake kubwa ni kubadilisha toka aya moja kwenda nyingine na pia hutumika kusogeza ukurasa au aya chini pale unapokibonyeza huku kasa ikiwa ipo kwenye aya hiyo.

        Kwa upande mwingine hutumika kukubali yaani pale unapotakiwa kutekeleza agizo au maelekezo fulani ukibonyeza kitufe hiki humaanisha ndiyo yani umekubali au umesema sawa kwa kile unachoulizwa.


    (2): Mausi/kiongozeo [Mouse]:

    Mausi ni chombo muhimu katika kompyuta ambacho hutuongoza na kutuonesha mahali tutakapoandika au kufanyia kitu chochote kwenye ukurasa tulio ufungua, hapa chini kuna maelezo ya matumizi yake kwa kina;

    Namna ya Kutumia Mausi/kiongozeo chako:
    [ How to use Your Mouse]:

    1. Kunavitufe viwili kwenye kila mausi/kionesheo. Ila kompyuta aina ya Apple inakuwa na kimoja tu na ambacho hutumika kama hizi nyingine kwa kubonyeza upande wa kushoto na kulia.

    2. Kitufe cha upande wa kushoto kwenye mausi/kiongozeo hutumika kufungulia programu na kuchagulia (to select items) maandishi au maneno au picha kwa ajili ya kuikopi, kukata au vinginevyo

    3. Kitufe cha upande wa kushoto hutumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kufanya.


    Kasa






    (3):Kipaza sauti: [Microphone]:


    Hiki katika kompyuta kurekodi sauti kwa ajili ya kuituma kama barua pepe au simu.

    (4):Skana/Scanner


    Hiki hutumika kubadili picha kutoka katika hali ya kawaida na kuinakili na kuifanya iwe katika mfumo wa kielektroniki na kuweza kutumwa kwa pamoja na barua pepe na pia kuweza kuhifadhiwa na kuonekana kwenye mdahalishi.

  2. Vifaa vya uendeshaji: [processing devices]:

    Sakiti/Circuit



    Hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho Central Processing Unit (C.P.U.). Mfano wake ni sakiti circuit; hiki huendesha na na kuunganisha pamoja habari na taarifa zote kwenye kompyuta.
  3. Vifaa vya Kuhifadhia/kuhifadhia [Storage devices]

    Vifaa hivi hutumiwa kwenye kompyuta kuhifadhi na kukumbuka habari mbalimbali

    (1): Flopi diski draivu/ Floppy disk drive (mara nyingi hujulikana kama A: draivu)



    Diski draivu hutumika kuingizia disketi ilkuhifadhia data au kazi za mtumiaji.

    Disketi ni kifaa kinachoondosheka/kubebeka na ambacho hutumiwa kunakilia na kuhifadhia data na kazi mbalimbali za watumiaji wa kompyuta.

    (2): CD Rom draivu /CD Rom disk drive.


    Hizi zina ni sehemu zinayotunza kumbukumbu za data mbalimbali (Memory).

    (3):Hadi diski Draivu/Hard Disk Drive

    Hii hujulikana zaidi kwa jina la Draivu "C" na kuwa inapatikana ndani ya kompyuta.

  4. Vifaa vya kutoa: [Output devices]

    (1):Skrini/kioo: [screen/monitor]:

    Hiki ni kioo cha kompyuta ambacho ndicho mtumiajia anachoangalia na kuyaona yale yote ambayo anayafanya kwa kutumia kompyuta yake.



    (2):Kichapishio: [printer]:

    Hiki hutumika kuchapishia kazi mbalimbali kutoka katika kompyuta.

    (3):Spika: [Speakers]:

    Hizi spika hutumika kusililizia muziki, maelezo na sauti mbalimbali toka kwenye kompyuta

    .

  5. Vifaa vya kuwasiliana [Communication Devices]



    (1): Kebo: [Cables]:

    Kebo hutumika kuunganishia kopyuta na vifaa vingine kwenye umeme



(2): Modemu: [Modem]:

Modemu hupatikana ndani ya kompyuta japo zamani zilikuwa nje ya kompyuta . Hii hutumika kuunganishia kompyuta kwenye mtandao wa mdahalishi.


[Rudi juu (Back to Top)][Rudi Nyuma (Back)Utangulizi]
[Endelea(Next)Windows1][Rudi Kwenye yaliyomo-Contents]

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni