MBEYA YETU YAPOKEA MSAADA WA MAFUTA KWA WALEMAVU WA NGOZI (ALBINO
Meneja masoko wa asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya nchini Czech ya Bez Mamy, Chris Lameck, akimkabidhi mafuta Jenga James Ambaye ni mlemavu wa ngozi |
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akimkabidhi Jenga James mafuta ya kutibu ngozi |
Jenga Jemsi(36) mkazi wa Songwe wilayani Mbeya alisema tangu amezaliwa hajawahi kupewa msaada wa mafuta licha ya kusikia kuwepo kwa mafuta mengi kwenye uongozi wa chama chao unaotolewa na watu mbali mbali.
Wananchi mbali mbali wa Nchi ya Jamhuri
ya Czech barani Ulaya wametoa msaada wa mafuta ya kutibu ngozi kwa ajili ya
watu wenye matatizo hayo(Albino) wa Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo
kwa mmiliki wa Mtandao wa Mbeya yetu, Meneja masoko wa asasi isiyokuwa ya
Kiserikali ya nchini Czech ya Bez Mamy, Chris Lameck, katika hafla iliyofanyika
katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, alisema msaada huo umetolewa na
wananchi na kuuwasilisha kwenye Asasi hiyo.
Alisema msaada huo hutokana na maombi ya
wahusika kutaka kusaidiwa baadhi ya vitu ambapo asasi hiyo hutangaza kwa
wananchi ambao hujitolea kadiri wanavyoguswa na asasi hiyo huvituma kwa
wahusika ambapo Mkoa wa Mbeya dawa hizo zimekabidhiwa kwenye ofisi za mtandao
wa www.mbeyayetu.blogspot.com
kwa ajili ya kuwafikishia wenye matatizo ya ngozi.
Mafuta yaliyokabidhiwa ni chupa kumi kwa
ajili ya watoto wadogo pamoja na chupa mbili kwa ajili ya watu wazima ambazo
alipewa Albino mmoja aliyejitokeza uwanja wa ndege kutokanana kuwa na mahitaji
makubwa baada ya ngozi yake kuharibika.
Akishukuru kwa msaada huo Jenga
Jemsi(36) mkazi wa Songwe wilayani Mbeya alisema tangu amezaliwa hajawahi
kupewa msaada wa mafuta licha ya kusikia kuwepo kwa mafuta mengi kwenye uongozi
wa chama chao unaotolewa na watu mbali mbali.
Kwa upande wake moja ya Wakurugenzi wa Mbeya yetu, Joseph
Mwaisango ametoa wito kwa wazazi wenye watoto walio na ulemavu wa ngozi kufika
ofisini kwake kuchukua mafuta hayo kwa kuwa ni machache kutokana na kuuzwa
gharama kubwa.
Mafuta hayo tunatoa bure.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni