Wednesday, June 4, 2014
BREAKING NEWS: MTOTO MCHANGA AOKOTWA KWENYE SHIMO IGANZO MBEYA , AFARIKI MUDA MCHACHE BAADA YA KUOKOLEWA.
Kichanga kikiwa kimefunikwa Baada ya kuokolewa na muda mchache kufariki
Shimo ambamo kichanga hicho kimekutwa
Mashuhuda wakishuhudia
Wengine wakiwa wameduaa
Watoto wakiwa wanatimuliwa eneo la tukio
****
WIMBI la wanawake mkoani Mbeya
kujifungua watoto na kisha kuwatupa na wengine kutoa mimba limezidi kushika
kasi na kukithiri baada ya vitendo hivyo kuripotiwa na vichanga kuokotwa kwenye
mashimo na mitoni.
Kukithiri kwa vitendo ni baada
ya leo Wananchi wa Mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya kugundua
kutupwa kwa mtoto anayesemekana kuwa na umri usiozidi siku moja jinsia ya kike
katika shimo la choo kisichotumika.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa
Mtaa huo, aliyefahamika kwa jina la Lukasi Mwakalonge, alisema alipewa taarifa
na wananchi wake mchana na kuambiwa kuna katoto kametupwa shimoni na bado ni
kazima hali iliyomlazimu kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi.
Alisema baada ya kufika eneo la
tukio na kugundua kuwa mtoto bado yuko hai wakaamua kumtoa ndani ya shimo huku
wakisubiri jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi lakini akawa amepoteza
maisha muda mfupi baada ya kutolewa ndani ya shimo.
Hata hivyo jeshi la Polisi
lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, vitendo hivyo vya
wanawake kutupa watoto kabla na baada ya kujifungia bado vinazidi kutokea hapa
nchini ingawa hakuna takwimu sahihi za wanawake waliopatikana na hatia kwa
makosa kama hayo.
NA CLEVER JULIUS
NA CLEVER JULIUS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni